Wednesday, August 15, 2007

JE WAMJUA JOACHIM MENANS MAZYETTA?

Huyu si mwingine ni yule ambaye anayeogopwa sana na wengi ila si tabia yake , mbaya bali kwa ucheshi aliokuwa nao, hasa kwa kuwachora watu vikatuni na vibonzo mbalimbali, Joachim ni mtu mmoja mwenye utani wa hali ya juu, asiyependa makuu, wala majivuno ,katika kazi zake za Usanii.

Katika maisha yake , amekumbana na mfumo wa maisha mengi.Joachim alizaliwa katika kijiji cha Sofi wilayani Ulanga , mkoanni Morogoro ,Tanzania.Amezaliwa mnamo tarehe 03.April. 1982 saa mbili usiku siku ya jumamosi.Baba yake ni Menans Joachim Mazyetta,na Mama yake ni Fransiska Frans Ngogo, Maisha ya wazazi wangu wote ni walimu , ila kwa mapenzi ya mwenyezi Mungu baba yangu alifariki mnamo tarehe 03.04.2005, katika hospitali ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro alikuwa AKISUMBULIWA NA MARADHI YA TB, MUNGU AILAZE MAHALA PEMA ROHO YAKE PEPONI AMINA.

1 comment:

ndeshiro said...

karibu kaka kwenye ulimwengu wa sayansi na tenkinolojia ufaidi matunda ya utanda wazi